Kuhusu EAGT SAYUNI

Kanisa la Sayuni -Sinoni Eagt Arusha.

Tunamshukuru Mungu kuwa kanisa letu limeendelea kukua kwa neema ya Mungu, Tangu pale watumishi wa Mungu walipoanza huduma yao katika mji huu wa Arusha mwazoni mwa miaka ya 90. Hadi sasa kanisa limekuwa kwa Idadi ya wanaookolewa kila siku.

Pia tumekuwa chimbuko la uenezaji wa makanisa ya EAGT katika mkoa wa Arusha ana mikoa yote jirani yaani Arusha Tanga na Kilimajaro na , na kwa sababu hiyo matokeo ya huduma hii ni dhahiri kwa jamii ya inayo tuzunguka, kwa taifa la Tanzania na nje ya mipaka ya nchi yetu.

Kanisa la Sayuni chini ya watumishi wa Mungu Dr Leonard Mwizarubi pamoja na mama linaamini katika “kuongeza thamani ya maisha ya watu” kupitia mafundisho sahihi ya neno la Mungu (Biblical based teaching)

Huu ndio umekuwa msingi mkubwa wa huduma ya ya watumishi hawa wa Mungu latika eneo hili la sinoni Unga limited Arusha, na jamii yote inayowazunguka.

Furaha yao imekuwa kuona Mungu anabadili historia za wanasayuni wote moja baada ya mwingine kwa utukufu wa Mungu. “1 Sam 22:2”

SERA YETU NI..

Utakatifu

Tunaamini kupitia mafundisho sahihi ya neno la Mugu na nguvu ya Roho mtakatifu mtu anaweza kuishi maisha matakatifu akiwa hapahapa duniani tofauti kabisa na fikra potofu kuwa haukuna utakatifu duniani    “Zab 16:3”

Maadili Yetu ya Msingi
Imani Yetu
Taarifa ya Mwaka